Skip to main content
Skip to main content

Viongozi wa Kakamega wataka serikali idhibiti wahuni wa kisiasa

  • | Citizen TV
    186 views
    Duration: 1:32
    Baadhi ya viongozi wa kaunti ya Kakamega wametaka vyombo vya usalama kuchukua hatua thabiti na za haraka kudhibiti uhuni katika ulingo wa siasa nchini. Akizungumza katika Kanisa la CITAM mjini Kakamega, Gavana wa Kakamega Fernandes Barasa alionya kuwa hali hiyo, ikiwa haitadhibitiwa, inaweza kulitumbukiza taifa kwenye ghasia. kadhalika alilaani vikali kisa ambacho wahuni walivamia seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi, na vile vile ghasia zilizoshuhudiwa katika mikutano ya viongozi wa upinzani eneo la Kikuyu.