- 2,654 viewsDuration: 3:06Viongozi wa kidini sasa wanasema wana wasiwasi kuhusu ongezeko la joto la kisiasa na utumizi wa makundi ya kihuni katika mikutano ya kisiasa nchini. Viongozi hawa kutoka sehemu tofauti nchini wanaonya kuwa msukosuko wa siasa za kihuni huenda ukatatiza amani ya nchi. Wakuu hawa wa makanisa pia wakishutumu vurumai la punde zaidi katika kaunti ya Kiambu ambako makundi ya wahuni yalionekana kujitokeza wakati wa mkutano wa upinzani.