Skip to main content
Skip to main content

Viongozi wa K.Kwanza wataka upinzani kumheshimu rais

  • | Citizen TV
    380 views
    Duration: 1:43
    Viongozi wa muungano wa Kenya Kwanza wameendelea kuwakosoa baadhi ya viongozi wa upinzani kwa kumkosea heshima Rais, wakisema matamshi yao ya hivi karibuni yamevuka mipaka ya staha ya kisiasa. Wakizungumza kwenye hafla ya kanisa eneo bunge la Nandi hills kaunti ya Nandi, walimnyoshea kidole cha lawama aliyekuwa Naibu Rais, Rigathi Gachagua, na kundi la viongozi wa upinzani wakiwahusisha na matukio ya uhuni yaliyojiri hivi karibuni. Walisema kuwa hafla za kitaifa kama mazishi zinapaswa kuheshimiwa na kutumiwa kuleta umoja badala ya kuwa majukwaa ya mashambulizi ya kisiasa.