Wabunge waitaka wizara wa Kilimo kuwahakikishia wakulima wa majani chai usawa kwenye malipo ya mazao

  • | Citizen TV
    29 views

    Wabunge wanaitaka wizara wa kilimo kuwahakikishia wakulima wa majani chai usawa kwenye malipo ya mazao yao. Wabunge hao wanaitaka mamlaka ya ustawi wa majani chai - KTDA - kusawazisha malipo ili wakulima katika maeneo ya bonde la ufa pia wafaidi. Haya ni huku KTDA ikisema kuwa itafanya mazungumzo na serikali ilikuleta usawa huo. Katibu katika wizara ya kilimo Dkt. Paul Rono hata hivyo amesema kuwa hana uwezo wa kuamua bei ya majani chai huku akiwataka wakulima kuhakikisha kuwa mazao yao yanafikia kiwango kitakachowahakikishia bei bora.