Wahudumu wa afya wahangaika kwa kukosa usafiri katika kaunti ya Busia

  • | Citizen TV
    187 views

    Maafisa wa afya wa nyanjani pamoja na wakunga katika kaunti ya Busia wanasikitika kuwa changamoto za usafiri zimechangia pakubwa akina mama wajawazito kujifungulia nyumbani. Wanawake wengi wajawazito katika kaunti ya Busia hutafuta huduma za wakunga, wakiamini kuwa huduma hizo zikiwemo kukandwa hurahisisha safari yao ya uja uzito, huku wakunga katika eneo hilo wakichukua jukumu la kuwapeleka wanawake hao hospitalini na kuwasajili.