Wakaazi wa kibokoni kaunti ya Kilifi walalamikia unyakuzi wa ardhi

  • | Citizen TV
    320 views

    Wakaazi wa Kibokoni na wadau katika sekta ya Utalii Malindi kaunti ya Kilifi wamelalamikia unyakuzi wa ardhi ya bahari na mabwenyenye ambao wanapania kujenga katika ardhi ilioachwa na bahari. Kulingana nao hatua hiyo imeathiri utalii na sasa wanataka hatua kuchukuliwa kwani hata mazingira ya bahari yameharibiwa na tinga zilizokata minazi,mikoko na baadhi ya miti iliyoko kando ya bahari.