- 304 viewsDuration: 2:05Mamia ya jamii ya Waislamu kutoka mtaa wa Kiamaiko hapa jijini Nairobi waliandamana barabarani wakidai kuwa ipo njama ya kunyakua ardhi ya msikiti wa Huruma. Kulingana nao, baraza kuu la Waislamu nchini SUPKEM lina mpango wa kujenga nyumba za biashara katika ardhi hiyo. Wanamtaka mwenyekiti wa kitaifa wa SUPKEM Hassan Ole Naado kulinda ardhi hiyo msikiti usibomolewe.