- 468 viewsDuration: 2:32KUMBUKIZI ZA JUNI 25 Viongozi wa kisiasa na maafisa wa serikali kutoka eneo la Nyanza wamewapongeza wakazi wa eneo hilo kwa kupuuza wito wa kushiriki katika maandamano ya siku ya Alhamisi. Wanasema kuwa hatua hiyo ilidhihirisha kuwa eneo liko tayari kwa maendeleo. Viongozi hao walio-kongamana huko Migori kwa ajili ya mpango wa uwezeshaji wa wanawake waliwataka wenyeji kumuunga mkono Rais William Ruto katika azma yake ya kuchaguliwa tena kwa minajili ya maendeleo endelevu. Kama Wycliffe Oketch anavyoripoti, wakazi wa eneo hilo walitakiwa kujiandikisha kwa wingi kuwa wapiga kura ili kulipa eneo hilo sauti inayohitajika kabla na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive