Skip to main content
Skip to main content

Watu wanaoshukiwa kuwa Al Shabaab waua walimu na chifu katika eneo la Hulugho, Garissa

  • | Citizen TV
    5,444 views
    Duration: 40s
    Watu wawili wameuawa kwenye shambulizi lililotokea katika eneo la Hulugho kaunti ya Garissa. Miongoni mwa waliouawa kwenye shambulizi hilo ni Chifu wa eneo la Hulugho Abdifatah Gani na Mwalimu Stephen Musili kutoka Shule ya msingi ya Hulugho. Inaripotiwa kuwa, wanamgambo wa Al Shabaab walivamia kijiji hicho ambako walimuua chifu na kisha kuchoma gari lake. Baadaye walifyatua risasi na kumuua mwalimu huyo aliyekuwa nje ya nyumba yake. Maafisa wa usalama eneo hilo wanasema wameanzisha operesheni kuwasaka wanamgambo hao