- 1,262 viewsDuration: 1:44Shuguli za masomo Katika shule ya msingi ya Kangai Mwea Kaunti ya Kirinyaga zilitatizika baada ya Wazazi waliokuwa na ghadhabu kuandamana kulalamikia gharama ya karo. Wakiwa wamebeba mabango na matawi, wazazi hao walivamia shule hiyo walimlaumu mwalimu mkuu kwa kuongeza karo. Wazazi hawa wakimlaumu mwalimu huyo kwa kile wanasema ni kuongeza mzigo wa karo licha ya elimu ya msingi kutangazwa kuwa bure na serikali. Waandamanaji waliingia kwenye madarasa ambapo wanafunzi walilazimika kuondoka madarasani.