Skip to main content
Skip to main content

Waziri Duale asema serikali haitalipa malipo ghushi ya SHA

  • | Citizen TV
    187 views
    Duration: 1:09
    Waziri wa afya Aden Duale amesisitiza kuwa mamlaka ya afya ya jamii SHA, haitalipa madeni ghushi kwa huduma ambazo hazikutolewa kwa wagonjwa na hospitali zinazodai mamlaka hiyo. Duale amesema madeni hayo lazima yafanyiwe ukaguzi wa kina ili kubaini uhalisi wake kabla ya malipo hayo kufanyika. Akizungumza mjini Garissa, Duale amesema mamlaka hiyo imelipa karibu bilioni 75 ikiwemo mpango wa afya ya wafanyikazi wa umma, huduma za dharura na hazina ya magonjwa sugu akitoa onyo kwa hospitali zinazolipisha huduma ya afya ya misingi kuwa zitachukuliwa hatua ya kisheria.