- 174 viewsDuration: 3:08Ni afueni kubwa kwa wakazi wa Muhonia, Laikipia ya Kati, baada ya serikali ya kaunti ya Laikipia kufungua zahanati katika eneo hilo, ambayo wamekuwa wakiisubiri kwa muda wa miaka 27. Wakazi hao wamesema kuwa hapo awali walikumbwa na changamoto kubwa za kupata huduma za matibabu kutokana na kutembea muda mrefu kutafuta huduma za afya.