
2,707 views
Watu 9 wafariki baada ya ndege kuanguka
Ndege binafsi ya biashara imeanguka katika mji wa Florida nchini Marekani, na kusababisha vifo vya watu tisa waliokuwa ndani ya ndege hiyo, kwa mujibu wa waziri wa uchukuzi wa Marekani. Ndege hiyo ilikuwa imetoka Austin, jimbo la Texas, na ilikuwa ikielekea Bahamas ilipoanguka umbali wa takriban maili tisa kutoka Mar-a-Lago, makazi ya Rais Donald Trump yaliyopo Florida. Uchambuzi wa data za safari ya ndege unaonesha kuwa ndege hiyo ilikuwa ikishuka kwa kasi ya mamia ya futi kwa sekunde kabla ya kuanguka. Hata hivyo, hakuna mtu aliyekuwa ardhini aliyejeruhiwa katika ajali hiyo. - - #bbcswahili #marekani #ajali Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw
- Wafanyakazi wakwama baada ya kufunikwa na theluji Japan
- Mitazamo ya dini kuhusu mwisho wa Dunia
- AMKA NA BBC - NOVEMBA 23' 2026
- Walimu 5 hatiani kwa kuwanyanyasa wanafunzi wa kiume kingono
- Wushu: Sanaa ya mapigano inayovutia vijana wa Kenya.
- ‘Tutakuwa na katiba mpya 2029’ asema Samia Suluhu Hassan. Katika Dira ya Dunia TV
- Matangazo ya Dira ya Dunia Redio 20/ 11 /2026
- Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan aahidi kuwepo kwa katiba mpya ifikapo mwaka 2029.