
11,918 views
MV Mwanza yagonga mwamba katika ziwa Victoria
Meli ya MV Mwanza imepoteza mwelekeo na kugonga miamba ya Bismarck wakati nahodha akifanya jitihada za kuitia nanga katika Bandari ya Mwanza, Ziwa Victoria. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, muda mfupi baada ya meli hiyo kugonga miamba, moshi mwingi ulianza kutoka, hali iliyosababisha taharuki miongoni mwa watu waliokuwa eneo hilo. Hata hivyo, hadi sasa hakuna taarifa zilizoripotiwa kuhusu watu kujeruhiwa kutokana na tukio hilo. Chanzo cha ajali hiyo na kiwango cha uharibifu wa meli bado havijafahamika. MV Mwanza ni miongoni mwa miradi mikubwa ya serikali katika kuboresha usafiri wa majini nchini Tanzania. Meli hiyo ilizinduliwa Januari, 2026, na Waziri Mkuu Dk Mwigulu Nchemba katika Bandari ya Mwanza Kusini. #bbcswahili #ajali #mvmwanza #ziwavictoria Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw
- Wafanyakazi wakwama baada ya kufunikwa na theluji Japan
- Mitazamo ya dini kuhusu mwisho wa Dunia
- AMKA NA BBC - NOVEMBA 23' 2026
- Walimu 5 hatiani kwa kuwanyanyasa wanafunzi wa kiume kingono
- Wushu: Sanaa ya mapigano inayovutia vijana wa Kenya.
- ‘Tutakuwa na katiba mpya 2029’ asema Samia Suluhu Hassan. Katika Dira ya Dunia TV
- Matangazo ya Dira ya Dunia Redio 20/ 11 /2026
- Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan aahidi kuwepo kwa katiba mpya ifikapo mwaka 2029.