
2,176 views
Watu 31 wafariki baada ya lori la mafuta kupinduka Cairo, Misri
Watu 31 wamefariki dunia na wengine 21 kujeruhiwa baada ya lori la mafuta kugongana na magari mengine na kusababisha moto mkubwa kwenye barabara yenye shughuli nyingi mjini Cairo, Misri. Hospitali za karibu zilipokea majeruhi waliokuwa na majeraha ya kuungua moto na matatizo ya kupumua kutokana na kuvuta moshi baada ya tukio hilo kutokea Jumatano jioni. Mamlaka bado hazijatoa maelezo rasmi kuhusu chanzo cha moto huo. Hata hivyo, vyombo vya habari vinavyomilikiwa na serikali vimeripoti kuwa lori hilo lilipinduka na kumwaga mafuta kwenye magari yaliyokuwa jirani, hali iliyochochea moto huo. #bbcswahili #misri #ajaliyamotomisri Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw
- AMKA NA BBC - NOVEMBA 27' 2026
- Matangazo ya Dira ya Dunia TV
- Seneta ahutubia bunge akiwa na mtoto
- Mwanamke ajitosa ndani ya gari la mgeni kujinusuru na bata mzinga
- Maandalizi kuelekea Afcon 2027 Afrika Mashariki
- AMKA NA BBC - NOVEMBA 26' 2026
- Matangazo ya Dira ya Dunia TV
- Matangazo ya Dira ya Dunia Redio 25/ 11 /2026