
21,502 views
Mitazamo ya jamii ya mimi kuwa dereva mwanamke bado ipo!
Monica Maduhu Makindi ni dereva wa lori ambaye licha ya kukutana na changamoto nyingi katika kazi yake, bado anakumbana na mitazamo ya watu wanaotilia shaka uwezo wake kwasababu tu ni mwanamke. Anasimulia tukio moja lililomtokea eneo la Igunga, alipowasimamisha na kuwapa lifti wanawake watatu waliokuwa na mtoto. Hata hivyo, mmoja wao alipogundua kuwa Monica ndiye aliyekuwa akiendesha lori, alikataa kupanda. Monica anasema tukio hilo lilimuumiza, hasa kwa kuwa nia yake ilikuwa kuwasaidia wanawake hao waliokuwa safarini usiku. Katika makala ya Waridi wa BBC, @Martha_Saranga anazungumza na @monicamaduhu163 kuhusu ubaguzi na mitazamo anayokutana nayo akiwa mwanamke katika sekta ya udereva wa malori. Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw
- Rwanda: Vijana wabuni vitambaa vya nguo kuupita migomba
- Wafanyakazi wakwama baada ya kufunikwa na theluji Japan
- Mitazamo ya dini kuhusu mwisho wa Dunia
- AMKA NA BBC - NOVEMBA 23' 2026
- Walimu 5 hatiani kwa kuwanyanyasa wanafunzi wa kiume kingono
- Wushu: Sanaa ya mapigano inayovutia vijana wa Kenya.
- ‘Tutakuwa na katiba mpya 2029’ asema Samia Suluhu Hassan. Katika Dira ya Dunia TV
- Matangazo ya Dira ya Dunia Redio 20/ 11 /2026