Makanisa zaidi yaikosoa mienendo ya serikali

  • | Citizen TV
    3,665 views

    Viongozi zaidi wa makanisa wamejitokeza kuikosoa serikali kwa kile inachosema ni kukosa uwajibikaji. Kanisa la kianglikana likisema linaunga mkono msimamo wa wenzao wa kanisa katoliki kuitaka serikali kupunguza maneno mengi bila vitendo. Aidha, makundi ya kidini kutoka Nyanza pia yameoa msimamo sawa, wakikemea kuzidi kwa ufisadi.