Mfumo wa kidijitali wa NEMIS kugeuzwa kuwa KEMIS huku serikali kuwasajili upya wanafunzi wote nchini

  • | Citizen TV
    483 views

    Serikali inapania kuwasajili upya wanafunzi wote nchini kwenye mfumo mpya wa kidijitali, KEMIS. Kuhamia kutoka kwa mfumo wa kidijitali wa sasa - NEMIS - kunasemekana kusababishwa na mapungufu ya mfumo huo na pia kuwezesha data yote ya wanafunzi kuhifadhiwa sehemu moja itakayotumiwa na kila mshika dau.