Baadhi ya wahudumu wa bodaboda nchini waanza kukumbatia matumizi ya pikipiki za elektroniki

  • | Citizen TV
    3,296 views

    Baadhi ya wahudumu wa bodaboda humu nchini wameanza kukumbatia matumizi ya pikipiki za elektroniki wakati ambapo serikali imetangaza mipango ya kuzindua pikipiki za umeme kufuatia ahadi ya rais william ruto wakati wa sherehe za madaraka mwaka huu. Wahudumu hao wa pikipiki, wamedokeza kuwa gharama yao sasa imepungua haswa wakati huu ambapo bei ya petroli imepanda. Ben Kirui alitangamana nao na hii hapa taarifa yake.