Naibu Rais Rigathi Gachagua aahidi kuleta mabadiliko ya kufanikisha kilimo cha kahawa

  • | Citizen TV
    328 views

    Naibu Rais Rigathi Gachagua ameahidi kuleta mabadiliko ya kufanikisha kilimo cha kahawa hapa nchini ili wakulima wapate malipo bora ya zao hili. Gachagua amesema haya alipoongoza kongamano la siku mbili na wadau katika sekta ya kahawa huko Meru kutafuta suluhu ya swala la malipo duni kwa wakulima ilhali kahawa ya hapa nchini ina sifa ya kuwa bora zaidi duniani.