- 444 viewsBaada ya kusafiri sehemu mbalimbali duniani kwa mwaka moja, Asami Okano, mwalimu wa Kijapani, alifanya makazi yake Uganda ili kuanzisha biashara ya kilimo cha kakao na vanilla. Hapa ndipo alipokutana na mume wake, Yoshito Asai, mwaka 2013. Walioana na kupata watoto wawili, wote walizaliwa Uganda. Mwandishi wa VOA Halima Athumani na Mukasa Francis walikutana na familia hiyo na wanasimulia hadithi yao kutoka wilaya ya Kayunga katikati mwa Uganda. Asami amesema, kama mwanafunzi, alikuwa na utashi wa kujifunza kuhusu nchi zinazoendelea, hususan Asia na Afrika. Hivyo basi, wakati wa ziara yake ya m waka mmoja, iliyompeleka katika nchi mbalimbali, aliwasili Uganda, na kupata kazi ya kujitolea katika kituo cha yatima. Alifanya kazi hapo kwa mwaka mmoja kabla ya kituo cha yatima kufungwa kutokana na ukosefu wa ufadhili. Bado akiwa nchini Uganda, Asami alifanya utafiti wa njia nyingine za kujipatia kipato na kugundua kilimo kama njia inayofaa. Aliamua kufuata mkondo huo na kufanya makazi yake Uganda. Yoshito alihamia Uganda kama msafiri, akifanya utafiti wake kuhusu kilimo, wakati akiwa pia anatafuta kazi huko. Akiwa katika harakati hizo, Yoshito alikutana na Asami, na kuajiriwa naye, kabla ya wote wawili kuamua kuoana na kuishi Uganda. Yoshito anasema kile hasa anachokipenda kuhusu nchi hiyo ni watu wake na hali ya hewa. #uganda #japan #cocoa #expats #africa #voa
Wanandoa wa Kijapani waeleza kilicho wavutia kutafuta maisha Uganda
- - Duniani Leo ››
- - Kenya-Finland Ties ››
- 14 May 2025 - Chairman Anangwe says the varsity should be allowed to function without threats.
- 14 May 2025 - The report highlights how employers subjected the women to extreme exploitation in private homes, often fuelled by racism.
- 14 May 2025 - The audit found that ministries, departments and agencies failed to provide documentation for Sh783.9 million in spending.
- 14 May 2025 - Presidential aspirants are focusing on the youth, as the 2027 general election battle shapes up.
- 14 May 2025 - NLC boss admitted that while the commission can investigate land grabs, it lacks authority to revoke illegal titles.
- 14 May 2025 - The commission said they need Sh3 billion to hire the interns on permanent and pensionable terms.
- 14 May 2025 - The government last week unveiled its leasing programme, handing over four public sugar factories to private players.
- 14 May 2025 - Safaricom CEO Peter Ndegwa has addressed concerns about the company's involvement in the Social Health Authority (SHA) system, clarifying that its role is limited to the digitisation of the process.
- 14 May 2025 - Sean "Diddy" Combs' former girlfriend, Casandra Ventura, the star prosecution witness at the hip-hop mogul's sex trafficking trial, testified on Tuesday that her music career began to suffer as she increasingly spent her time participating in days of…
- 14 May 2025 - Senators yesterday put Kericho Governor Dr Eric Mutai on the spot over stalled Early Childhood Development and Education (ECDE) classroom projects, some of which have remained incomplete since the onset of devolution. This even as the lawmakers…