Rais Ruto atangaza nyadhifa za mawaziri kuwa wazi

  • | KBC Video
    153 views

    Rais William Ruto amechapisha kwenye gazeti rasmi la serikali arifa ya kuvunja baraza lake la mawaziri na kumteua wazii mwenye mamlaka makuu Musalia Mudavadi aliyepia waziri wa masuala ya kigeni kushikilia nyadhifa zote za mnawaziri. Kwenye arifa hiyo ya tarehe-12 Julai mwaka huu, rais Ruto amesema nyadhifa-21 za mawaziri na mwanasheria mkuu sasa ziko wazi. Rais amesema anafanyia mageuzi serikali yake ili kufanikisha utoaji huduma na kubuni baraza jipya la mawaziri hivi karibuni ambalo litamsaidia kutekeleza ajenda za serikali zikiwemo kudhibiti deni la kitaifa, kuimarisha mapato, kubuni ajira, kukomesha utumizi mbaya wa raslimali na urudufishaji majukumu miongoni mwa mashirika ya serikali.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive