- 251 viewsMawaziri wa jumuiya ya afrika mashariki wameidhinisha mpango wa pamoja wa kuufuatilia, kudhibiti na kuzuia kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola katika viwanja vya ndege, bandari na mipaka ya ukanda wa afrika mashariki. Mpango huo uliafikiwa kwenye mkutano wa dharura wa mawaziri wa afya kuhusu udhibiti wa ebola. Aidha mawaziri hao wa waliafikia kuunda kamati ya kiufundi ya kuratibu mikakati ya pamoja ya kukabiliana na ugonjwa huo.