- 1,333 viewsTume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi nchini imekamata Afisa Mkuu wa Maendeleo na Mipango ya Mijini Kaunti ya Nairobi, Patrick Analo, baada ya kupatikana na shilingi milioni 65.3 zinazodaiwa kufichwa nyumbani kwake. EACC inasema Analo na maafisa wengine ambao wangali kukamatwa wanachunguzwa kwa madai ya ubadhirifu wa mamilioni ya pesa za kaunti.