- 601 viewsFamilia ya mshukiwa mmoja wa mauaji ya Shakahola aliyefariki katika Hospitali ya Makadara inadai hawakufahamishwa kuwa jamaa yao alikuwa akiugua ugonjwa wa ini. Kelvin Sudi Asena alifariki akipokea matibabu. Familia yake inasema imeachwa kwenye njia panda baada ya kukabidhiwa mwili kwa mazishi huko Vihiga. Na kama anavyoarifu Francis Mtalaki, familia hiyo inataka majibu kuhusu watoto watano ambao hadi sasa hawajulikani waliko licha ya kutoa sampuli za DNA miaka mitatu iliyopita.