Kesi ya kubanduliwa kwa gavana wa Isiolo Abdi Guyo

  • | Citizen TV
    145 views

    Kesi ya kubanduliwa kwa gavana wa Isiolo Abdi Guyo itasikizwa jumanne tarehe 8 na jumatano tarehe 9 mwezi Julai, maseneta wote wakitarajiwa kuwa na kikao maalum cha kuamua hatma ya gavana huyo. Guyo anakabiliwa na tuhuma za ukiukaji wa katiba, akiwaajiri washauri 36 na maafisa 31 wa wizara licha ya kaunti hiyo kuwa na wizara 6 tu. Gavana huyo pia ametuhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha za basari za wanafunzi za kima cha shilingi milioni 30. Waakilishi wadi wa isiolo walimbandua gavana huyo Alhamisi tarehe 26 mwezi Juni