Kundi la wanawake wanaoishi na virusi vya ukimwi Machakos watafuta mbinu za kujiimarisha kimaisha

  • | K24 Video
    151 views

    Kundi la wanawake wanaoishi na virusi vya ukimwi katika kaunti ya Machakos limetaja mshikamano wao kama moja ya sababu kuu za wao kujiimarisha kimaisha. Kundi hilo lenye zaidi ya wanawake ishirini linasema mikutano yao ya mara kwa mara imewasaidia wengi kufuatilia matibabu kwa makini na hata kuanza mipango ya kujikuza kiuchumi. Wanawake hao kutoka eneo la mitaboni wanahisi unyanyapaa ungali changamoto kwa watu wanaoishi na virusi hivyo.