Mlipuko wa Kipindupindu Wazua Hofu Nairobi, Kisumu na Migori

  • | K24 Video
    183 views

    Mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu umeripotiwa katika kaunti za Nairobi, Kisumu na Migori, huku Wizara ya Afya ikithibitisha visa 97 na vifo sita. Katika maeneo yaliyoathirika, wahamasishaji wa afya ya jamii wameitaka serikali kuongeza rasilimali ili kudhibiti maambukizi, hasa kwenye mitaa ya mabanda ambako upatikanaji wa maji safi ni changamoto kuu.