- 205 viewsAfisi ya msajili wa vyama imeonya dhidi ya kubuniwa kwa vyama vya kisiasa visivyo na misingi imara na ambavyo hutumiwa wakati wa uchaguzi pekee. Akizungumza jijini Kisumu, msajili wa vyama John Cox Lorionkou alisema kuwa afisi yake inapiga msasa vyama thelathini vinavyopania kuingia katika orodha rasmi ya vyama vya kisiasa nchini. Msajili huyo pia amewataka Wakenya kushiriki katika uundaji wa vyama ili kuimarisha demokrasia.