Skip to main content
Skip to main content

Ruto atetea karantini ya Ebola Laikipia, ashukuru Marekani kwa ufadhilI

  • | Citizen TV
    1,249 views
    Rais William Ruto ametetea vikali mpango wa kujenga Kituo cha Karantini ya Ebola kwa Wamarekani katika kambi ya kijeshi huko Laikipia, akisema kwamba Marekani imefadhili mpango huo kwa shillingi billioni 1.8 inayotumika vile vile kujenga maeneo 23 ya karantini nchini. Akizungumza nchini Afrika Kusini, Rais Ruto amesema kuwa kuwepo kwa karantini kama hivyo nchini kutawafaidi watu wote kwnai ugonjwa wa ebola haubagui kwa misingi ya uraia. Rais Ruto anasema Kenya inafaa kurejesha mkono kwa marekani kutokana na ufadhili wa miaka mingi katika sekta ya afya.