- 1,549 viewsDuration: 3:45Rais William Ruto leo alilihutubia Bunge la Tanzania, Dodoma, kuhusu mradi wa kusafisha mafuta aliousema unatarajiwa kuanzishwa mkoa wa Tanga, Tanzania. Rais Ruto alisema kiwanda hicho kitatoa nafasi za ajira na kupunguza bei ya mafuta Afrika Mashariki. Hata hivyo, alijikuta katika hali ya utata hapo jana baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kusema hajui lolote kuhusu mradi huo unaokadiriwa kugharimu zaidi ya shilingi trilioni 2.5.