- 884 viewsDuration: 1:44Serikali kuu na ile ya kaunti ya Kwale zimetakiwa kukarabati na kuimarisha barabara za eneo la Shimba Hills ambazo ziko katika hali mbaya hususan wakati huu wa mvua. Mwenyekiti wa chuo cha Bandari Maritime Lung'anzi Mangale Chai, amesema eneo hilo linategemewa pakubwa kwa uzalishaji wa chakula na hivyo ukosefu wa barabara huwasababishia wakulima na wafanyibiashara hasara kubwa.Aidha wakaazi wa Kwale wameraiwa kuwapiga msasa wanasiasa kabla ya kuwapigia kura ili kuhakisha wanawachagua viongozi watakaoleta maendeleo mashinani.