- 629 viewsImani ya Wakenya kwa Rais William Ruto inazidi kushuka huku utafiti wa shirika la TIFA ukionyesha kuwa asilimia 68 ya Wakenya hawana imani naye. Kwa mujibu wa utafiti huo, Wakenya pia wamekosa imani na taasisi muhimu za serikali, zikiwemo idara ya polisi, bunge na IEBC. Zaidi ya theluthi mbili ya Wakenya wanaamini nchi inaelekea pabaya huku gharama ya maisha ikizidi kupanda na hali ya uchumi ikiendelea kuwa ngumu.