Jioni hii inabainika kuwa baadhi ya wanafunzi walioahidiwa nafasi za shule ya sekondari ya juu bila karo wala sare hawakuendelea na masomo. Baadhi ya wanafunzi hao kutoka mtaa wa Mukuru hapa Nairobi wanasema walifukuzwa shule siku chache baada ya kupelekwa na maafisa wa serikali. Ufichuzi huu umejitokeza siku moja baada ya ripoti ya Baraza la Mitihani la KNEC kuonyesha kuwa zaidi ya wanafunzi laki moja na nusu hawakuendelea na masomo ya mpito wa CBE. Hata hivyo, Katibu wa Elimu, Julius Bitok, amesema ripoti hiyo si ya kweli.