Vurugu Zabisha Bunge la Machakos, Spika Asitisha Vikao Vyote

  • | K24 Video
    12 views

    Mvutano mkali umezuka leo katika Bunge la Kaunti ya Machakos, na kusababisha majeraha kwa baadhi ya wawakilishi wadi. Ghasia zilianza baada ya makundi mawili ya MCAs kukabiliana kuhusu hatma ya Spika Ann Kiusya — kundi moja likimtetea, huku jingine likitaka aondolewe. Mzozo huo uliendelea hadi jioni, na kulazimu Spika kujifungia ofisini mwake. Kupitia taarifa rasmi kwa vyombo vya habari, Spika ametangaza kusitishwa kwa vikao vyote vya Bunge hadi atakapotoa tangazo jipya.