Skip to main content
Skip to main content

Wizara ya Elimu yaagiza ukaguzi wa shule za bweni nchini

  • | Citizen TV
    124 views
    Wizara ya Elimu imeamrisha ukaguzi wa shule za bweni kote nchini ili kuhakikisha usalama wa wanafunzi. Katibu katika wizara hiyo, Julius Bitok, amesema tayari wameongeza maafisa wa ubora wa elimu ambao wanatarajiwa kutoa ripoti ndani ya siku kumi. Katibu huyo amewataka viongozi wa shule kujadiliana na wanafunzi akiongeza kuwa kalenda ya shule haitabadilishwa na likizo fupi itasalia tarehe ishirini na nne mwezi huu.