- 133 viewsWizara ya Elimu sasa inasema inataka pesa zilizoagizwa kufadhili masomo zizingatiwe kwenye bajeti kikamilifu. Katibu katika wizara hiyo, Julius Bitok, amesema kuwa kwa sasa kuna upungufu wa fedha za elimu ambao huenda ukalemaza idara ya elimu. Katika bajeti hiyo, Bitok anasema kuwa kuna upungufu wa zaidi ya bilioni 100 ambao anataka Wizara ya Hazina ya Kitaifa kuuangazia kabla ya wiki ijayo ya bajeti kusomwa.