
58,417 views
Paul Mackenzie, amehukumiwa kifungo cha miaka 200 jela
Kiongozi wa kanisa la dhehebu tata nchini Kenya, Paul Mackenzie, amehukumiwa kifungo cha miaka 200 jela na Mahakama Kuu ya Mombasa kwa mauaji ya watu 191, wote isipokuwa mmoja wakiwa watoto. Mackenzie pamoja na wafuasi wake zaidi ya 20 walikutwa na hatia ya kuendesha mfumo uliopangwa ndani ya Msitu wa Shakahola, ambapo waliwaelekeza wazazi kuwanyima watoto wao chakula hadi kufa, wakidai kwamba walikuwa wakifanya hivyo ili “wakutane na Yesu.” Mackenzie, aliyejitambulisha kama mchungaji, alikamatwa mwaka 2023 baada ya kugunduliwa kwa zaidi ya miili 400 katika makaburi yasiyo na kina ndani ya Msitu wa Shakahola, karibu na pwani ya Kenya. Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw
- Matangazo ya Dira ya Dunia TV
- Kigogo mwingine wa dawa za kulevya anaswa na FBI
- Rwanda: Vijana wabuni vitambaa vya nguo kuupita migomba
- Wafanyakazi wakwama baada ya kufunikwa na theluji Japan
- Mitazamo ya dini kuhusu mwisho wa Dunia
- AMKA NA BBC - NOVEMBA 23' 2026
- Walimu 5 hatiani kwa kuwanyanyasa wanafunzi wa kiume kingono
- Wushu: Sanaa ya mapigano inayovutia vijana wa Kenya.