
20,978 views
Jinsi mtego wa mapenzi ulivyovunja mtandao CIA nchini Ghana
Kwa miongo kadhaa, mashirika ya kijasusi yamekuwa yakitumia mbinu inayojulikana kama sexpionage au honey trap yaan kutumia mahusiano ya kimapenzi kumshawishi mtu kufichua taarifa za siri. Mojawapo ya visa vilivyoacha alama kubwa katika historia ya ujasusi wa Marekani kilitokea Accra, nchini Ghana, wakati wa Vita Baridi. @frankmavura anasimulia kisa cha Sharon Scranage, mfanyakazi wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) ambaye alitumia nafasi yake kazini kufichua taarifa nyeti kwa mpenzi wake Michael Soussoudis aliyekuwa na uhusiano na idara ya usalama ya Ghana. Taarifa hizo zilisababisha kufichuliwa kwa majasusi na watoa taarifa wa CIA, kuvuruga shughuli za shirika hilo nchini Ghana na kuhatarisha mtandao wake wa ujasusi katika eneo hilo la Afrika. #bbcswahili #ujasusicia #ghana Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw
- Mchungaji anayetoa mahubiri ya kupotosha nchini Nigeria.
- Matangazo ya Dira ya Dunia TV
- Kigogo mwingine wa dawa za kulevya anaswa na FBI
- Rwanda: Vijana wabuni vitambaa vya nguo kuupita migomba
- Wafanyakazi wakwama baada ya kufunikwa na theluji Japan
- Mitazamo ya dini kuhusu mwisho wa Dunia
- AMKA NA BBC - NOVEMBA 23' 2026
- Walimu 5 hatiani kwa kuwanyanyasa wanafunzi wa kiume kingono