
845 views
Mwanaume na mbwa wake wasombwa na mawimbi makali ya bahari
Tazama mwanaume huyu na mbwa wake walivyonusurika kusombwa na maji ya bahari kutokana na mawimbi makubwa yaliyosababishwa na hali ya maji kujaa kupita kawaida katika ufukwe wa Cannon Beach, jimbo la Oregon, Marekani. Tukio hilo lilitokea wakati wa kile kinachoitwa King Tides, kipindi ambacho maji ya bahari hupanda na kufikia viwango vya juu sana kuliko kawaida. Hata hivyo, mwanaume huyo na mbwa wake waliokolewa bila kupata madhara, kwa mujibu wa polisi. Mamlaka zimewaonya watu kuepuka kwenda ufukweni kutokana na mawimbi makubwa, maji ya bahari kufurika na mafuriko ya maeneo ya pwani yanayoathiri sehemu za pwani magharibi ya Marekani. #bbcswahili #marekani #kingtides Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw
- Viongozi waliobadili katiba kubaki madarakani.
- AMKA NA BBC - NOVEMBA 27' 2026
- Matangazo ya Dira ya Dunia TV
- Watu 31 wafariki baada ya lori la mafuta kupinduka Cairo, Misri
- Seneta ahutubia bunge akiwa na mtoto
- Mwanamke ajitosa ndani ya gari la mgeni kujinusuru na bata mzinga
- Maandalizi kuelekea Afcon 2027 Afrika Mashariki
- AMKA NA BBC - NOVEMBA 26' 2026