
22,140 views
Apata watoto wanne kwa pamoja akiwa na miaka 50
Jamii mara nyingi huwawekea wanawake matarajio kuhusu umri ambao wanapaswa kupata mwenza, kuolewa na kuwa mama. Lakini kwa Olusola Olonade, maisha yalichukua mwelekeo tofauti. Alifunga ndoa akiwa na umri wa miaka 48 na miaka miwili baadaye, akiwa na miaka 50, akajifungua watoto wanne mapacha kupitia teknolojia ya urutubishaji wa mayai nje ya mwili (IVF). Simulizi yake ni ya imani isiyoyumba, uvumilivu na fursa zinazotolewa na maendeleo ya teknolojia ya uzazi. Sasa akiwa na furaha ya kuwapokea watoto wake wanne wachanga, Olusola tayari anatazama mbali zaidi ya maisha ya sasa. Kwa matumaini makubwa, anasema anaamini ataishi kuwaona watoto wake wakikua na siku moja hata kuwa nyanya wa vitukuu vyake. 🎥: @mobolaji Olatunde Watayarishaji: Annette Arotiba na Ahmed Ambali Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw
- Kigogo mwingine wa dawa za kulevya anaswa na FBI
- Rwanda: Vijana wabuni vitambaa vya nguo kuupita migomba
- Wafanyakazi wakwama baada ya kufunikwa na theluji Japan
- Mitazamo ya dini kuhusu mwisho wa Dunia
- AMKA NA BBC - NOVEMBA 23' 2026
- Walimu 5 hatiani kwa kuwanyanyasa wanafunzi wa kiume kingono
- Wushu: Sanaa ya mapigano inayovutia vijana wa Kenya.
- ‘Tutakuwa na katiba mpya 2029’ asema Samia Suluhu Hassan. Katika Dira ya Dunia TV