- 25,709 viewsDuration: 4:19Huzuni na Majonzi zilihanikiza katika makafani ya hospitali ya rufaa ya Naivasha ambapo familia za wanafunzi 16 waliofariki kwenye mkasa wa moto katika bweni la shule ya wasichana ya Utumishi zilipokezwa matokeo ya vipimo vya msimbojeni na kuona mabaki ya miili ya wana wao. Familia moja iliruhusiwa kuchukua mwili kwa mazishi kulingana na dini ya kiislamu. Hata hivyo familia 15 zilizosalia zitalazimika kusubiri zaidi huku serikali ikipanga ibada ya pamoja ya wafu kabla ya kuruhusiwa kuwazika wapendwa wao.