Kidagaa kimemwozea Chiloba

  • | KBC Video
    17 views

    Mkurugenzi mkuu wa Halmashauri ya mawasiliano humu nchini aliyesimamishwa kazi, Ezra Chiloba anakabiliwa na hali ngumu. Kidagaa kilimwozea Chiloba alipojipata akiondoka katika afisi ya tume huru ya uchaguzi-IEBC kwa mtindo sawa na huo. Na jinsi ilivyokuwa katika tume ya IEBC alipotuhumiwa kwa kashfa za ununuzi vifaa vya uchaguzi mkuu wa 2017, Chiloba anakabiliwa na tuhuma kadhaa zikiwemo utumizi mbaya wa shilingi milioni 662 za mikopo ya ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wa Halmashauri ya Mawasiliano uliosababisha asimamishwe kazi mara moja. Abdiaziz Hashim anaripoti.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channe: l: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive