Ukumbusho wa waliofariki Sunbeam wafanywa Nairobi

  • | Citizen TV
    452 views

    Huku dhiki ikizidi kuwakumba waathiriwa wa maandamano, hafla ya maombi ya ukumbusho wa watu watatu waliouwawa katika duka la kibiashara la sunbeam imefanyika leo jijini nairobi. Wafanyibiashara waliokuwa wakifanya kazi katika jumba hilo lililoporwa na kuteketezwa wakati wa maandamano walijumuika na wajane na jamaa za walioaga dunia kwenye hafla iliyosheheni machungu na majonzi tele.