Baadhi ya shule zimeanza kuwatuma wanafunzi nyumbani baada ya mgomo wa KUPPET kuzidi wiki mbili

  • | Citizen TV
    404 views

    Huku mgomo wa walimu wa shule za upili KUPPET ukiingia wiki ya pili hii leo, baadhi ya shule zimeanza kuwatuma nyumbani wanafunzi.

    Katika kaunti ya Nakuru, shule ya wasichana na ile ya wavulana ya Jomo Kenyatta zimewaagiza wanafunzi kurejea nyumbani hadi mgomo wa waalimu utakapokamilika. Wazazi waliofika shuleni mapema leo walisema wamepokea ujumbe uliowataka kufika shuleni kuwachukua watoto wao. Masomo katika shule za upili za umma hayajaendelea huku walimu nao wakishikilia kuwa hawatarejea kazini hadi mwajiri wao TSC itakaposikilizwa matakwa yao.