Watoto 465,000 Makueni kuchanjwa dhidi ya magonjwa

  • | Citizen TV
    149 views

    Watoto elfu 465 kaunti ya Makueni wanatarajiwa kupata chanjo dhidi ya ugonjwa kipindupindu na ukambi baada ya magonjwa hayo kuongezeka katika kaunti ya Makueni. Zoezi la kutoa chanjo hiyo limeongozwa na mke wa gavana wa Makueni Anita Mutula katika shule ya msingi ya Unoa ambapo ilibainika kuwa visa vitatu vya ugonjwa wa ukambi viliripotiwa Makueni mwaka uliopita na chanjo hii ni afueni katika juhudi za kukabiliana na magonjwa hayo