Wazazi wazuiliwa kuingia katika shule ya Upper Hill baada ya ripoti za mlipuko wa kipindupindu

  • | Citizen TV
    271 views

    Zogo limeshuhudiwa nje ya shule ya Upper Hill hapa Nairobi, baada ya wazazi kufika shuleni humo kutaka maelezo zaidi kuhusiana na mlipuko wa kipindupindu shuleni humo. Kufika kwa wazazi kumefuatia ripoti kuwa watoto kumi na sita bado wanapokea matibabu kufuatia kipindupindu huku wengine 95 wakitibiwa na kuruhusiwa kuondoka hospitali.