Wakulima katika eneo la Taita wataka mashine za kukaushia nafaka

  • | Citizen TV
    209 views

    Wafanyibiashara wa mahindi eneo bunge la Taveta kaunti ya Taita Taveta wanaitaka serikali ya kitaifa kupitia wizara ya kilimo kuhakikisha mashini za kukausha mahindi zinapatikana sehemu hiyo. Wafanyibiashara hao ambao huagiza mahindi kutoka nchi jirani ya Tanzania wanasema mara kwa mara mahindi yao hukosa kukauka kwa wakati kutokana na ukosefu wa mashini hizo. Kadhalika wanasema kuna haja kwa mataifa ya Kenya na Tanzania kuondoa vikwazo vingi vya uaguzaji wa mahindi mpakani