Wawakilishi wadi wakutana baada ya Guyo kuponea shoka

  • | Citizen TV
    515 views

    Wawakilishi wadi wa Bunge la Kaunti ya Isiolo jana walifanya kikao chao cha kwanza tangu jaribio la kumbandua Gavana Abdi Ibrahim Guyo kupitia hoja ya kumwondoa madarakani. Kikao hicho kimefanyika juma moja baada ya bunge la seneti kutupilia mbali hoja ya kumuondoa Gavana guyo kwa misingi ya dosari za kisheria, baada ya Bunge la Kaunti kushindwa kuthibitisha kuwa kulikuwa na kikao halali cha kuwasilisha hoja na hatimaye kumbandua